Home Simba SC ISHU YA MABEKI WA SIMBA KURUDIA MAKOSA ITARUDISHA MABAO MATANOTANO KIMATAIFA

ISHU YA MABEKI WA SIMBA KURUDIA MAKOSA ITARUDISHA MABAO MATANOTANO KIMATAIFA


Anaandika Saleh Jembe

 WAKATI fulani huwa nawasikia baadhi ya viongozi hata mashabiki wakiwatuhumu baadhi ya wachezaji wao kuuza mechi.


Mara nyingi ukitaka uthibitisho huwa hakuna zaidi ya kuelezewa namna wachezaji walivyoacha kukaba na kutoa nafasi kwa wapinzani kufunga bao, kusababisha faulo na kadhalika.

Inawezekana haya mambo yapo kwa kuwa Waswahili wanasema lisemwalo lipo.

Pamoja na hivyo, mimi huamini kumekuwa na mengi sana ya kiufundi ambayo yanawalazimisha baadhi ya viongozi na mashabiki kuamini ni tatizo la kuuza mechi.

Mfano mzuri ni mabao mawili katika mechi ya Simba ikicheza dhidi ya wenyeji wake, Dodoma Jiji pale jijini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Bao la kwanza la Simba, kichwa huru kutoka kwa  Kagere akiwa katikati ya mabeki lakini angalia Dodoma Jiji walivyosawazisha kwa kichwa huru katikati ya mabeki wa Simba.

Mabeki hao wa Simba wanaocheza michuano ya kimataifa, walirudia kosa lilelile dakika ya mwisho ya mchezo kuruhusu mchezaji apige kichwa huru na Manula akawa nwokozi wao.

Onyo kwa Simba, kama mabeki wao watakubali kuruhusu makosa yanayofanana na haya katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hakika Al Ahly na wengine hawatawaacha na huu ndio uitakuwa mwanzo wa kurudi zile 5 tena.

Katika mechi na Dodoma Jiji, mabeki wa Simba wamefaya kosa hili mara 3. Moja Dodoma wakakosa, 2, likawa bao na 3, Manula kafanya ya ziada lakini Vs Al Ahly, AS Vita au Al Merreikh, INAWEZEKANA ZOTE MABAO.


Safu ya mabeki wa Simba inaongozwa na nyota Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa, wengine ni Kened Juma, Ibrahim Ame.
SOMA NA HII  SIMBA HUYU NI MTU SIO MALAIKA.... MSIJIJAZE UPEPO