Home Yanga SC YANGA:HATUNA PRESHA, TUTAPAMBANA KUFIKIA MALENGO

YANGA:HATUNA PRESHA, TUTAPAMBANA KUFIKIA MALENGO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo imara hauna presha katika kutimiza jambo lao la kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu wa 2020/21 ulio mikononi mwa Simba.

Jana ilikuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na iligawana pointi mojamoja.

Bao la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 84 lilionekana kulalamikiwa na wachezaji wa Mbeya City huku lile la kuweka usawa kwa Mbeya City lilifungwa dakika ya 90+3 na Athas Pastory kwa mkwaju wa penalti ambao ulilalamikiwa na wachezaji wa Yanga.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri kwa msimu huu wa 2020/21 hivyo mashabiki wasiwe na presha.

“Tupo imara hatuna presha katika yale ambayo tunayafanya, imani 

yetu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mechi zetu zilizobaki na kupata pointi tatu muhimu.“Kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi limekubaliana kufanya kazi kwa juhudi hicho ndicho ambacho tunakifanya kwa sasa ndani ya uwanja,” amesema.

Yanga imekusanya jumla ya pointi 45 ipo nafasi ya kwanza na imecheza jumla ya mechi 19, Mbeya City ipo nafasi ya 17 na ina pointi 15 baada ya kucheza jumla ya mechi 19. 

Ikiwa imefunga jumla ya mabao 30, Michael Sarpong ametupia mabao manne, Wazir Junior ametupia bao moja huku Saido Ntibanzokiza akiwa ametupia mabao mawili.

Kinara wa utupiaji ni Deus Kaseke mwenye mabao matano ndani ya Yanga inayonolewa na Cedric Kaze.

SOMA NA HII  KISA OFA YA WAARABU....MAYELE AIPA MASHARTI MAGUMU YANGA...ATAKA MSHAHARA MKUBWA ZAIDI...