Yanga SC

FISTON ATAMBA YANGA KUMALIZA SARE MFULULIZO

admin February 16, 2021 12:47 pm

  MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, FISTON Abdoul Razack, ametamba kuwa anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika michezo iliyo mbele yao na kumaliza tatizo la matokeo ya sare mfululizo.

Nyota huyo alisajiliwa na kikosi cha Yanga katika kipindi cha dirisha dogo, ambapo mpaka sasa ameichezea Yanga michezo miwili akiwa bado hajafunga bao lolote. 

Akizungumzia malengo yao Fiston amesema:”Kila mmoja amesikitishwa na matokeo tuliyopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, na tumedhamiria kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika michezo yetu ijayo kwa kuwa malengo yetu ni kutwaa ubingwa,”

Yanga kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza dhidi ya Kagera Sugar, ambapo matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda kwa bao 1-0.


CARLINHOS ATAJA SABABU ZA KUTOKUCHEZA YANGA NAMUNGO: WAANGOLA WALITUFANYIA UHALIFU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply