Home Simba SC TSHISHIMBI – KWA SIMBA HII…WASHINDWE WENYEWE TU KWENDA ROBO FAINALI

TSHISHIMBI – KWA SIMBA HII…WASHINDWE WENYEWE TU KWENDA ROBO FAINALI


KIUNGO Mkongomani wa AS Vita, Papy Kabamba ‘Tshishimbi’ amekiri kwamba, kwa jinsi SImba ilivyo imebadilika kwa kiwango kikubwa kuliko misimu misili iliyopita, imebaki kwao tu kupenya kundini kwenda robo fainali Ligi ya Mabingwa.

Nyota na nahodha huyo wa zamani wa Yanga, alisema Simba ya sasa imeongezeka ubora kutokana na wachezaji wengi kuwa katika kiwango kizuri ambacho kinaweza kushindana na timu yoyote.

“Unajua kwa upande wetu AS Vita hatukuwa na maandalizi mazuri ya kwenda kukabiliana nao, timu iliyokuwa sawa kama Simba ambao wanaweza kupata pointi moja ugenini jambo ambalo si rahisi katika mashindano haya kupata pointi tatu ugenini,” alisema.

“Simba hawakutuzidi katika maeneo mengi, ila wanacheza kimbinu zaidi wanakaba na kushambulia kwa pamoja, lakini ubora wa uamuzi wa mchezaji mmojammoja ulichangia kwa kiasi mikubwa kufanya kwao vizuri.”

Kiungo huyo aliyewahi kukipiga Mbabane Swallows, alisema mara kadhaa amekuwa akikutana na Simba hufanya mazoezi na kujiandaa vya kutosha, lakini mara hizi mbili za mwisho wamenikuta nikiwa katika wakati mgumu na kupata wakati mgumu mbele yao.

“Mara ya kwanza ilikuwa katika mechi ya Dar es Salaam, nikiwa na Yanga tulifunga mabao 4-1 katika nusu fainali ya Kombe la FA, nilikuwa nimetoka katika majeraha sikuwa fiti na utimamu wa mwili. Safari hii pia nimefanya mazoezi na timu kwa muda wa wiki baada ya kutoka katika karantini ya siku 14, sikuwa na ufiti wa kutosha kushindana dhidi ya viungo wao,” alisema.

Naye kocha msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu aliyewahi kuinoa Yanga na kushiriki nayo mechi za makundi ya mwaka 1998, alisema Simba imekuwa bora zaidi ya walivyokutana mara ya mwisho msimu uliopita na kushinda 5-0 jijini Kinshasa.

SOMA NA HII  JE SIMBA WATAENDELEZA UBABE LEO!?