MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa tatizo kubwa ambalo linaikumba timu yake ni umaliziaji wa nafasi ambazo wanazitengeneza ndani ya uwanja.
Kwa sasa Arsenal inajiandaa na mchezo wao wa kesho, Februari 25 wa hatua ya 32 bora dhidi ya Benfica kesho ambayo ni ya Ligi ya Europa.
Ikiwa Uwanja wa Emirates, Februari 21 iliruhusu kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Artreta amesema:”Tatizo kubwa kwa timu kwa sasa lipo kwenye umaliziaji kwani wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia ndani ya uwanja.
“Hilo nimeliona na tumefanyia kazi. Tunajua kwamba tuna mchezo mgumu na kwetu itakuwa ni kama fainali hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri,” .
Arsenal watacheza nchini Ugiriki katika Jiji la Athens wakiwa nyumbani baada ya taifa la England kukataa mechi hiyo isipigwe nchini kwao kutokana na kuamini kwamba Ureno kuna Corona nyingi hivyo wachezaji wa Benfica wangekwenda kuliongeza janga hilo.