BAADA ya Waarabu wa Misri Al Ahly kufungwa bao 1-0 mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Pitso Mosimane amesema kuwa hawajafungwa kwa mbinu bali hali ya hewa haikuwa rafiki kwao.
Bao la ushindi kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa lilipachikwa kimiani na Luis Miquissone dakika ya 30 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 jambo lililowamaliza wapinzani hao.
Mosimane amesema:”Tulikuwa tunajitahidi namna ya kwenda na wapinzani wetu na hili tulijua tangu awali jambo ambalo lilitufanya nasi tuongeze juhudi ndani ya uwanja.
“Kwa kilichotokea wanapaswa wapewe pongezi ila hatujapoteza kwa ajili ya mbinu zaidi ilikuwa ni hali ya hewa ambayo haikuwa rafiki kwetu.
“Muda wa jioni kwetu si rafiki hivyo tumejitahidi kwa namna ambavyo tumeweza tukashindwa kupata matokeo,hivyo mazingira hayakuwa rafiki kwetu, bado tuna kazi mbele na bado tuna mechi hivyo hatujakata tamaa,”.
Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, Al Ahly hawakuwa na muda wa kubaki ndani ya ardhi ya Tanzania walikwea pipa na kurejea nchini Misri.