kimataifa

POGBA BADO SANA NDANI YA MANCHESTER UNITED

admin February 26, 2021 6:47 am

PAUL Pogba, kiungo wa Klabu ya Manchester United anatarajiwa kuendelea kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja kwa kuwa yupo kwenye hali ya kurejea kwenye ubora wake kutoka kwenye majeraha aliyopata.

Wakati Manchester United ikilazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Real Sociedad kwenye mchezo wa Europa League, jana hakuwa sehemu ya kikosi kilichoanza.

Pogba alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Everton ambao ulikuwa ni wa Ligi Kuu England na ulikamilika kwa sare ya kufungana mabao 3-3, Februari 6 baada ya kupata maumivu ya nyama za paja.

Tayari amekosekana kwenye mechi tatu katika mashindano yote chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer ambaye anapambana kumsaka mbadala wa Mfaransa huyo mwenye mbwembwe nyingi akiwa ndani ya uwanja.

Solkjaer amesema:”Paul bado hajawa fiti na atakuwa nje kwa wiki kadhaa mpaka pale atakapokuwa imara.

Pia kwa sasa kocha huyo anasubiri taarifa njema kuhusu kurejea kwa nyota wake ambao wamekosa nao michezo mitatu ambao ni Scott Mc Tominay, Edinson Cavan na Donny van de Beek ambao nao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha.

 

AZAM FC HESABU ZAO NI KWA MBUNI SAIDO APONA, ATIMKIA BURUNDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply