Home Yanga SC ALICHOSEMA SENZO KUHUSU SAKATA LA MORRSON KUJIUNGA SIMBA

ALICHOSEMA SENZO KUHUSU SAKATA LA MORRSON KUJIUNGA SIMBA


MWAKA jana Yanga ilipeleka malalamiko yao CAS juu ya usajili wa mchezaji Bernad Morrison kwenda Simba haukufuata taratibu.

Morrison aliingia kwenye mgogoro na waajiri wake hao wa zamani ambao kabla ya kwenda CAS malalamiko yao yalianza kusikilizwa kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliyo chini ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) iliyoamua Morrison ni mchezaji huru kutokana na mapungufu yaliyokuwemo kwenye mkataba baina yake na Yanga.

Mwanaspoti linafahamu Januari mwaka huu Yanga ililipa Dola 24000 za Kimarekani (Sh54 mil) CAS ili kuanza kusikilizwa kesi hiyo pesa ambayo imeelezwa ilitakiwa ilipwe na pande zote mbili, Morrison na Yanga.

Akifafanua juu ya hilo, Mshauri wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa alisema;

“Tayari tumepangiwa hakimu wa kusikiliza kesi hiyo ambayo itaanza kusikilizwa muda wowote kwani pesa imelipwa, hicho kiasi kilipaswa kulipwa pande zote mbili.”

“Baada ya kuona upande wa pili umekataa kulipa tuliamua kulipa kiasi chote ili kesi isikilizwe maana tunahitaji haki itendeke juu ya usajili wake kwenda Simba ambao haukufuata taratibu,” alisema Senzo.

Kuhusu mchakato wao wa mabadiliko, Senzo alisema; “Kabla hatujapeleka kwenye matawi kwa wanachama wetu tutaanza kupeleka serikalini ili wapitie kama nyaraka ziko sawa ama kuna sehemu ya kurekebisha tuifanye kabla ya kupeleka kwa wanachama.”

SOMA NA HII  KOFFI OLOMIDE AWASILI BONGO, APOKELEWA NA HAJI MANARA