Home Uncategorized RUVU SHOOTING NI BALAA, WAPANIA KUUPIGA MBELE YA POLISI TANZANIA KAMA BARCELONA

RUVU SHOOTING NI BALAA, WAPANIA KUUPIGA MBELE YA POLISI TANZANIA KAMA BARCELONA


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa watawafudisha soka wapinzani wao Polisi Tanzania kwenye mchezo wao wa Lgi Kuu Bara utakaochezwa kesho Uwanja wa Ushirika Moshi.

Bwire amesema kuwa ushindi wa kibabe mbele ya Coastal Union wa mabao 2-1 ni salamu tosha kwa wapinzani wao Polisi Tanzania.

“Tupo Bongo ila tunapiga mpira kama Barcelona sasa unadhani tukikuana na Polisi Tanzania nini kitatokea? Tutawapigia mpira mwingi mpaka watasahau shida zao na kuanza kutushangilia sisi.

“Tunahitaji pointi tatu huu ndio mpango wetu mkubwa mengine yatatokea ndani ya uwanja, mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA WAAMUZI ITAFUTIWE DAWA MAPEMA, TIMU ZIJIPANGE KIUKWELI