Home Ligi Kuu COASTAL UNION YALIPA KISASI KWA KUINYOOSHA AZAM FC,KIGONYA AMPATA SHUJAA MPYA

COASTAL UNION YALIPA KISASI KWA KUINYOOSHA AZAM FC,KIGONYA AMPATA SHUJAA MPYA

 KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na George Lwandamina leo Februari 11 kimepoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union kwa kufungwa mabao 2-1.

Haji Ugando nyota wa Coastal Union alikuwa wa kwanza kumtungua mlinda mlango wa Azam FC, Mathias Kigonya,’Mikono Mia’ kwa mkwaju wa penalti dakika ya 9.

Daniel Amoah aliweka usawa bao hilo dakika ya 34 na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo ubao wa pale Tanga ukisoma 1-1.

Bao la ushindi kwa Coastal Union ya Juma Mgunda lilipachikwa dakika ya 54 na Rajab Majimengi na kuwafanya Azam FC wasiwe na mengi ya kufanya ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga hivyo leo Coastal Union wamelipa kisasi kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex,  Coastal Union ilifungwa mabao 2-0.

Shujaa wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Kigonya ambaye aliokoa penalti ya Clatous Chama Uwanja wa Mkapa leo ameshindwa kuokoa penalti ya shujaa Ugando wa Coastal Union. 

Ushindi huo unaifanya Coastal Union kufikisha jumla ya pointi 23 ipo nafasi tisa huku Azam FC ikibaki na pointi zake 33 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 19.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA YA LIGI BONGO LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here