Home Ligi Kuu HONGERA ISSA NGOAH,KAZI BADO NZITO KWA WANA IHEFU

HONGERA ISSA NGOAH,KAZI BADO NZITO KWA WANA IHEFU


ISSA Ngoah nyota anayekipiga ndani ya Ihefu FC kazi yake imeonekana ndani ya Ihefu kwa kutimiza majuku yake ndani ya uwanja kwenye mechi mbili mfululizo aliazoana kikosi cha kwanza.


Ngoah ameweza kuipa pointi nne timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila na amefunga jumla ya mabao matatu katika mechi mbili alichoza kwenye mzunguko wa pili.

Kwa sasa inapambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja kwa kuwa tangu mzunguko wa kwanza unaanza mpaka umemeguka haijawahi kuingia ndani ya 10 bora kwenye msimamo.

Ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza jumla ya mechi 20 na imekusanya jumla ya pointi 17.

Ngoah ameweza kuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga kwenye mechi mbili mfululizo ndani ya ligi jambo ambalo kwa Watanzania huwa ni nadra sana na kama inatokea huwa ni mara moja kisha inapotea jumlajumla.

Kwenye mzunguko wa pili jitihada zake na namna ambavyo anashirikiana na timu anastahili hongera ila kazi  bado ipo kwenye kutimiza majukumu yake pamoja na ya timu kiujumla.

Aina ya mabao pamoja na ufungaji anaonesha ana kitu hivyo anapaswa asivimbe bali aendelee kupambana, mabao matatu ndani ya mechi mbili ni kazi kubwa ambayo ameanza kufanya mzunguko wa pili.

Alianza mbele ya Ruvu Shooting mabao mawili kisha Mtibwa Sugar akawafunga bao moja, kila  la kheri mpambanaji.


SOMA NA HII  COASTAL UNION LEO KUONA MECHI YA MWISHO JERO TU