Home Yanga SC INGIZO JIPYA YANGA HATIHATI KUIVAA MBEYA CITY

INGIZO JIPYA YANGA HATIHATI KUIVAA MBEYA CITY


BEKI wa kati  Dickson Job ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kuna hatihati ataukosa mchezo wa kwanza kwenye mzunguko wa pili dhidi ya Mbeya City kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


 Licha ya kwamba ameanza mazoezi mepesi ndani ya timu yake mpya baada ya kusaini dili la miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar nafasi yake ya kuwapa  Mbeya City bado ndogo kwa kuwa  ana tatizo la nyama za paja.


Ikiwa ataukosa mchezo huo kwa msimu wa 2020/21 jumla atakuwa amewakosa Mbeya City mara mbili kwa kuwa hata alipokuwa Mtibwa Sugar Kwenye mechi zote 17 alikuwepo kikosi cha kwanza ila mchezo wa Mbeya City alikosekana.

Hafidh Saleh, meneja wa Yanga amesema kuwa Job amepewa program maalumu itakayomrejesha kwenye ubora.

“Alikuja akiwa ni majeraha hivyo ameanza program maalumu taratibu atarejea kwenye ubora na atajiunga na wenzake, “.

SOMA NA HII  HATIM AWASHAURI JAMBO HILI YANGA UPANDE WA KOCHA