Home Azam FC NADO: UKITAKA KUWAFUNGA SIMBA FANYA HIVI

NADO: UKITAKA KUWAFUNGA SIMBA FANYA HIVI


KIUNGO mshambuliaji wa kikosi cha klabu ya Azam, Idd Selemani Nado ‘Idd Nado’ amefunguka kuwa namna rahisi ya kuwafunga Simba ni kufanya maamuzi ya haraka mbele ya safu yao ya ulinzi ambayo mara kwa mara hufanya makosa.

Nado alihusika katika mabao yote mawili waliyoyapata katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba, katika mchezo wao wa kiporo uliopigwa siku ya Jumapili.

Akizungumzia mapungufu ya safu ya ulinzi ya Simba Nado alisema: “Simba ina wachezaji wengi bora ikiwemo mabeki wao hasa wa pembeni, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’.

“Hivyo kama utahitaji kupata matokeo dhidi yao ni lazima uhakikishe unakuwa na maamuzi ya haraka dhidi yao pale wanapofanya makosa.

Sare hiyo ya Jumapili iliwafanya Azam kufikisha pointi 33 katika michezo yao 18 waliyocheza hivyo kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo.

SOMA NA HII  MATAJIRI AZAM FC WAPANGA KUITIBULIA SIMBA DILI LA KUMRUDISHA ADEL...WAMFUATA NA MKATABA MNONO...