Home Habari za michezo KWA KUNDI HILI LA YANGA KWELI MBOGA MOTO UGALI MOTO

KWA KUNDI HILI LA YANGA KWELI MBOGA MOTO UGALI MOTO

Habari za Yanga

Mechi mbili zijazo kwenye kundi (D) zitatoa mwanga utakaoonesha timu zipi zina nafasi kubwa ya kutinga robo fainali CAF champions league 23/24.

Yanga walianza ratiba yao kwa mtego kwenye kundi (D). CR Belouizdad ugenini, Al-Ahly nyumbani. Point 1 sio mbaya wala nzuri kwa ratiba hiyo.

Turning point ya Yanga wakijipanga vyema huenda ikaanzia hapa :

Medeama vs Yanga

Yanga vs Medeama

Al-Ahly vs CR Belouizdad

CR Belouizdad vs Al-Ahly

◉ Yanga anahitaji kushinda dhidi ya Medeama home & Away ili kufikisha points (7). Wakati huo yeye akifikisha points (7), Waarabu ambao ndio wapinzani wagumu watakuwa wanauana wao kwa wao.

◉ Baada ya mechi hizo mbilimbili kupita, Yanga atabaki na mechi (1) dhidi ya CR Belouizdad nyumbani kwa Mkapa.

Akichukua points (3) kwa CR Belouizdad na kufikisha (10) taa ya kijani Kuelekea Robo

fainali CAF champions league itawaka

◉ Kinyume chake, hesabu zitakuwa ngumu sana kutinga robo fainali. Yote yako mikononi mwa Yanga kwani bado kuna points (12) za kugombea mpaka sasa.

So far, hata Wydad Athletic ambaye hana point katika michezo (2) ananafasi ya kutinga robo fainali. Bado ni asubuhi.

SOMA NA HII  RAIS AL-NASSIR AJUTA KUMSAJILI RONALDO..."NIMEUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA