Home Habari za michezo BAADA YA KUYEYUSHA DK 540 ZA CAF BILA LOLOTE…BENCHIKHA KUWASHUSHIA DAWA HII...

BAADA YA KUYEYUSHA DK 540 ZA CAF BILA LOLOTE…BENCHIKHA KUWASHUSHIA DAWA HII SIMBA..

Habari za Simba

Simba imetimiza dakika 540 ikicheza mechi sita za michuano ya kimataifa msimu huu bila kuonja ushindi, kitu ambacho hakijawahi kutokea kwao, lakini benchi la ufundi la timu hiyo limetuliza mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kwa kuwaambia watulie, kwani mambo mazuri yanakuja.

Simba ililazimishwa suluhu ugenini na Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mechi ya pili ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni muendelezo wa mdudu wa sare baada ya awali kutoka sare ya 2-2 kisha 1-1 na Power Dynamos ya Zambia mechi za mchujo.

Pia ilitoka sare ya 2-2 kisha 1-1 mbele ya Al Ahly ya Misri katika African Football League na wiki iliyopita ilibanwa tena na ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwenye mechi ya makundi.

Rekodi zinaonyesha Simba haijawahi kucheza mechi mfululizo kwa idadi kama hiyo bila ushindi, lakini kocha mpya, Abdelhak Benchikha amesema sare waliyopata ugenini sio mbaya sana, kwani bado lina nafasi ikizitumia mechi nne ilizonazo kundini.

Mchezo wa juzi ulikuwa wa kwanza kwa Benchikha tangu ajiunge na Simba akichukua nafasi ya Roberto Oliveira ‘Robertinho’ aliyetimuliwa baada ya kichapo cha 5-1 kutoka kwa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu ya Novemba 5.

Benchikha alisema kuwa suluhu hiyo haijaathiri mipango yao.

“Hatukupata muda wa kutosha kutengeneza timu, lakini tulipambana na kulinda heshima. Tunashukuru tumepata alama moja, sio mbaya. Bado tuna mechi za kufanya vizuri,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA vs AL HILAL....MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA LEO NI HAYA....