Home Uncategorized SADIO MANE NI BALAA TUPU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND

SADIO MANE NI BALAA TUPU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND

SADIO Mane, nyota wa timu ya Liverpool amefikisha jumla ya mabao 100 ndani ya Ligi Kuu ya England.

Mane alifikisha bao hilo kwenye mechi dhidi ya Norwich alipopachika bao 1 la ushindi na kuipa pointi tatu timu yake.

 Bao hilo alifunga akitokea benchi na kuwafanya wafikishe jumla ya pointi 76 kwenye ligi wakiwa nafasi ya kwanza na mabingwa watetezi Manchester City wapo nafasi ya pili wakiachwa kwa jumla ya pointi 25.

Endapo Liverpool itashinda mechi zake tano zinazofuata ndani ya ligi kati ya 13 watatangazwa kuwa mabingwa bila kujali matokeo ya timu nyingine.

SOMA NA HII  KOCHA AMPELEKA HAALAD APELEKWA REAL MADRID