Home Uncategorized AZAM FC:LIGI NGUMU KWELI

AZAM FC:LIGI NGUMU KWELI



OBREY Chirwa, mshambuliaji namba moja ndani ya Azam FC amesema kuwa Ligi Kuu Bara ya msimu huu 2019/20 ni ngumu jambo linalowafanya nao wapambane kupata matokeo.


Chirwa amefunga jumla ya mabao nane ndani ya ligi akiwa ni kinara wa kutupia kwa timu ya Azam FC.

“Ligi ni ngumu na kila timu inapambana kutafuta matokeo chanya jambo linalotufanya tupambane kutafuta ushindi, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 22.
SOMA NA HII  KAZI IMEANZA CAFCL WAPINZANI WA YANGA WAMTIMUA KOCHA WAO