Home Habari za michezo GAMONDI AFICHUA SIRI YA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NDANI

GAMONDI AFICHUA SIRI YA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI ZA NDANI

Habari za Yanga

KOCHA mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amefichukua  licha ya kucheza michezo ya ndani ya kirafiki lakini bado hajapata muunganiko mzuri kwa wachezaji wake akiwemo kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli na mshambuliaji wa   Hafiz Konkoni kabla ya kuana msimu mpya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Gamondi ametoa kauli hiyo baada ya Yanga kucheza michezo miwili ya kirafiki ambapo mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya Friends Rangers na kuibuka na ushindi wa mabao  huku ikitoka sare na JKU ya Zanzibar katika michezo ambayo imechezwa kwenye Uwanja wao wa mazoezi, Avic Town Kigamboni.

Yanga wanatarajia kuondoka kesho (Jumatatu) kuelekea Tanga katika michuano ya Ngao ya Jamii ambapo watacheza mchezo wao dhidi ya Azam, utakaopigwa Agosti 9, mwaka huu katika uwanja wa Mkwakwani.

Kocha Gamondi licha ya kupata matokeo na mazuri ndani ya kikosi chake lakini bado hajapata muunganiko wa wachezaji wapya ndani ya kikosi hicho hali inamyolazimu kutenga muda zaidi kwa ajili ya wakujenga wachezaji hao ili kuweza kufikia malengo ya timu hiyo.

Alisema anaendelea  vizuri na maandalizi ya kuelekea katika mashindano maalum ya Ngao ya Jamii  Tanga, wachezaji wapo katika hali nzuri kwa kuzingatia michezo ya kirafiki waliocheza imempa picha halisi ya muelekeo wa kikosi chake kuelekea msimu mpya.

“Sina shida ya uwezo wa wachezaji   kwa sasa nahitaji muda zaidi wa kuendelea kutengeneza muunganiko wa timu hasa kwa wachezaji wapya  bado hawafikia katika usawa na wale ambao walikuwepo ingawa tunamatarajio makubwa ya kuweza kufika mbali, ” alisema Gamondi.

Aliongeza kuwa  baada ya michezo hiyo miwili sasa anaendelea kukinoa kikosi chake kwa kuwapa program maalumu kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii ambayo itakuwa na changamoto kubwa kwa sababu ya matokeo yao ya kufanya vizuri kwa msimu uliopita.

SOMA NA HII  WAKONGO WAMGOMBEA NABI....AITELEKEZA YANGA UWANJA WA NDEGE