Home Habari za michezo TAMASHA LA SIMBA LAILETA TIMU HII BONGO

TAMASHA LA SIMBA LAILETA TIMU HII BONGO

KUELEKEA Kilele cha siku ya tamasha la Simba inafanyika leo, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi wanashuka dimbani kuwakaribisha Power Dynamos ya Zambia, ikiwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni sehemu ya kuwatambulisha wachezaji wale wa msimu uliopita na wale wapya waliosajiliwa msimu wa 2023/24 wa mashindano mbalimbali ikiwemo Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika tamasha la leo kutakuwa na wasanii mbalimbali  muzuki  akiwemo Khalid Ramadhani (Tunda Man), Oscar Lello (Whozu), Mwalimi Sadiki (Meja Kunta), (Tommy Flovour) , Twanga Pepeta na  Ally Saleh (King Kiba)  wataimba nyimbo maalum kuhusu Simba.

Mbali na burudani hizo pia kutakuwa na mechi maalum  za timu ya vijana na Simba Queens  wakishuka dimbani nao kucheza mechi ya kirafiki nao watakuwa sehemu ya utambulisho na   mechi malum ya wadhamini wa klabu hiyo kati ya Bank ya CRDB na NMB ambapo

Kwenye tamasha hilo Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ataunga na watanzania elfu 60,000 kushuhudia tukio hilo ambalo limekuwa na kivutio kikubwa hali iliyopelekea siku tatu kabla ya tukio kumaliza tiketi.

Kitendo cha kumalizika kwa tiketi mapema , uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa  mageti yanafunguliwa saa 2:00  badala ya 5:00 asubuhi ambapo mashabiki watapata burudani kuanza muda huu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally aliwataka mashabiki wasiopata tiketi watulie nyumbani na kutotokea uwanjani.

“Wanayekuja  kwa Mkapa mwenye uhakika wa tiketi, waliochelewa kupata tiketi wasisogee uwanjani kwa sababu usalama ni mzuri na kila sehemu ya uwanja itakuwa na Polisi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Raia,” alisema Ahmed.

Kuelekea mchezo huo dhidi ya Power Dynamos, Kocha wa Simba Roberto Oliviera (Robertinho) alisema  siku muhimu kwa mashabiki wa timu hiyo, wamejiandaa kukamilisha siku kwa kuwapa burudani.

Alisema Power Dynamos ni timu kubwa, anaamini kitakuwa kipino kizuri kwa wachezaji wake kuelekea katika mashindano yote ya msimu ujao.

“Tunakwenda kuonesha mchezo mzuri mbele ya mashabiki wetu, wachezaji wako tayari kwa mechi hiyo na zilizopo mbele yao  anamatarajio makubwa na nyota wake baada ya kukaa nao kambini kwa wiki mbili.

Watafanya  vizuri,  kikosi bora na chenye ushindani, naweza  kuchezesha vikosi viwili na akapata matokeo kutokana na uwezo wa kila mchezaji,” alisema Robertinho.

Nyota mpya wa timu hiyo, Che Fondoh Malone, alisema anashukuru kuwepo katika klabu hiyo, anawaahidi furaha mashabiki wa timu hiyo.

“Ninawafahamu Power Dynamos ni moja ya timu bora Afrika, tumejiandaa kufanya vizuri tunakwenda kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema nyota huyo.

Kocha wa Power Dynamos, Mwenya Chipepo alisema anafurahi kuwa sehemu ya sherehe za siku muhimu na timu kubwa ya Simba, anaamini utakuwa mchezo wa ushindani kwa sababu wanatumia mechi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Alisema wanakutana na timu kubwa yenye uzoefu wa mashindano ya kimataifa, yenye wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi jambo ambalo atapata nafasi kubwa ya kuona mapungufu ya kikosi chake kabla ya kuelekea kwenye mashindano ya kimataifa.

“Hii mechi kwetu ni mzuri kwa sababu tunaenda kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo uttanipa mwanga wa kuona mapungufu yetu na kuyafanyia kazi kabla ya kucheza michuano hiyo.

Kuhusu mashabiki wengi kuwepo uwanjani kwetu ni faida kubwa, ninaimani tunapata uzoefu kwa kuwa tutarejea tena kucheza na Simba baada ya kufanya vizuri katika mchezo wetu wa awali dhidi ya Afrika Stars,” alisema Kocha huyo wa Power Dynamos.

@@@@@@

SOMA NA HII  SAKATA LA HAJI MANARA NA BABBARA, SIMBA WATOA TAMKO