Home Habari za michezo KAZI IMEANZA CAFCL WAPINZANI WA YANGA WAMTIMUA KOCHA WAO

KAZI IMEANZA CAFCL WAPINZANI WA YANGA WAMTIMUA KOCHA WAO

Klabu ya CR Belouizdad ya nchini Algeria imethibitisha kumfuta kazi Kocha wake mkuu, Sven Vandenbroeck kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo wa kikosi hicho katika ligi kuu ya nchi hiyo.

Imeelezwa kuwa, Sven ambaye ni raia wa Ubelgiji, amepisha kauli na uongozi wa klabu hiyo hasa kuhusu mtazamo wa kimbinu wa kuifundisha timu hiyo.

Taarifa klabu hiyo leo Oktoba 8, 28023 imebainisha kuwa:- “Mwenyekiti wa Bodi ya vijana ya CR Belouizdad, Mahdi Rabhi, amesitisha mkataba wa kocha wa Ubelgiji “Svan Vandenbroek” kwa makubaliano ya pande zote na kumuondoa kwenye benchi la ufundi la timu kutokana na utofauti wa kimtazamo kati ya pande zote.”

Belouizdad iko nafasi ya 11 kwenye Ligi ya Algeria ikiwa imecheza michezo miwili, imeshinda mmoja na kufungwa mchezo mmoja baada ya jana kupoteza nyumbani mbele ya Kenchela FC. Belouizdad kwenye Ligi imefunga mabao 3 na kufungwa mBao 3

Ikumbukwe kuwa, Sven amewahi kuifundisha vilabu vya Simba SC ya Tanzania, FAR Rabat ya Morocco kabla ya kutimkia Wydad Casablanca ambako alidumu takribani moezi miwili ru na kutimuliwa ndipo akajiunga na Belouizdad.

CR Belouizdad ambayo anaichezea Simon Msuva (winga qa zamani wa Yanga), ni wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa kundi moja (Kundi D) pamoja na Medeama ya Ghana na Al Ahly ya Misri ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo.

Yanga itaanzia ugenini kwenye michuano hiyo ambapo watawafuata CR Belouizdad mnamo Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutupa karata yao ya kwanza kwenye hatua ya makundi ikiwa ni miaka 25 imepita tangu waingie hatua hiyo.

SOMA NA HII  WAKATI MOTO WA USAJILI YANGA UKIZIDI KUNOGA....MSUVA ABAKISHWA DAR KILAZIMA...AWEKEWA MEZANI MILIONI 150...