Home Habari za michezo GAMONDI AGÒMA KUZUNGUMZIA MECHI ZA KIMATAIFA AFUNGUKA HAYA

GAMONDI AGÒMA KUZUNGUMZIA MECHI ZA KIMATAIFA AFUNGUKA HAYA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema hataki kuongea lolote kuhusu mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, badala yake ameweka wazi  akili yake ipo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Azam FC, Oktoba 25.

Amesema baada ya kufanikiwa kupata alama tatu ugenini na Geita Gold FC nguvu zao wanazielekeza kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC , kwani wakati wa kuzungumzia mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, haujafika.

Yanga inatarajia kucheza dhidi ya Azam FC Oktoba 25, mwaka huu na kutumia mechi hiyo kama maandalizi ya michezo ya Ligi ya Afrika ambapo wamepagwa kundi D, zikiwemo na timu ya Al Ahly (Misri), Medeama (Ghana) na CR Belouizdad (Algeria).

Gamond alisema baada ya kuvuna alama tatu mbele ya Geita Gold FC sasa wanarejea uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na kujiandaa kwa mechi ijayo dhidi ya Azam FC.

Alisema muda huu hafikirii mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Afrika, zaidi ya kufanyia kazi kikosi chake kwa ajili ya mechi yao ijayo ya ligi kuu dhidi ya Azam FC ambayo itakuwa ya ushindani kwa sababu ya kila mmoja anahitajj kupata matokeo chanya.

“Kwa sasa tunaangalia mechi iliyopo mbele yetu, tunafanya kazi mechi baada ya mechi, nimeona kundi lakini kabla ya kukutana na timu hizo tunakibarua kigumu cha kutafuta pointi kwenye ligi ya nyumbani dhidi ya Azam FC.

Kundi ngumu ukiangalia timu zote ni bora kwa sababu ya kuzifahamu kasoro Medeama sijaijua vizuri, kwa sasa tunaangalia kilicho kuwa mbele yetu,” alisema Gamond.

Aliongeza kuwa amefurahishwa na kiwango kilichoonyesha na wachezaji wake walijua kutumia nafasi walizopata na kufanikiwa kuondoka na alama tatu dhidi ya Geita Gold FC.

Alisema wanarejea uwanja wa mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata anaimani kuba siku 10 za kujiandaa dhidi ya Azam FC licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Kuhusu kupoteza mechi na Ihefu FC, alisema wachezaji walikuwa na fatiki kutokana na wiki moja kucheza mechi tatu na kulazimika kufanya mabadiliko ya kikosi tofauti na mpinzani wao huyo alipata muda mrefu wa kujiandaa.

“Kupoteza mechi mmoja haina maana tumepoteza malengo yetu, ligi ndio imeanza kuna mechi nyingi mbele yetu na lolote linawez kutokea, kwa sababu kufungwa na sare ni mambo ya kawaida katika mpira,” alisema kocha huyo.

Kuhusu mchezaji wake Max Nzengeli alisema ni mchezaji mzuri na anafanya majukumu yake vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzake na kupata matokeo mazuri.

Naye Nzengeli alisema kazi yake ni mpira na atapambana kushirikiana na wachezaji wenzake wanapigania timu kupata matokeo mazuri ili kufikia malengo yao.

Alisema wamejipanga vizuri kusonga mbele katika kila mashindano ili kufikia malengo yao iwe ligi ya ndani kutetea mataji yao na michuano ya kimataifa kufikia mbali ikiwemo robo au nusu fainali

“Sipendi kuahidi bali nitafanya kazi kufikia malengo yetu, mashabiki wajitokeze kwa wingi  kuendelea kusapoti timu yao kila inapokuwa na kufikia malengo,”alisema nyota huyo.

Upande wa mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kikosi kimerejea salama na kupata mapumziko mafupi na kuingia kambini kujiandaa na mechi ijayo.

“Metacha (Mnata) na Jonas (Mkude) hawakuwa sehemu ya mipango ya mechi hizi mbili kwa sababu waliopata changamoto za kifamilia na taarifa zao kocha anaweza kuziweka wazi,” alisema Mratibu huyo.

SOMA NA HII  WYADAD WAPANGA KUMNG'OA LAKRED SIMBA....OFA ALIYOPEWA NI MO DEWJI TU ANAWEZA KUOKOA JAHAZI...