Home Habari za michezo JEMEDARI SAIDI:- SUALA LA CHAMA, SIMBA WALITUDANGANYA….?..

JEMEDARI SAIDI:- SUALA LA CHAMA, SIMBA WALITUDANGANYA….?..

Habari za Michezo leo

Tarehe 21 Desemba 2023 Sekretarieti ya Klabu ya Simba kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wake (CEO) ilitoa taarifa kwa umma kwamba klabu yao imewasimamisha wachezaji Clatous Chama na Nassoro Kapama kutokana na utovu wa nidhamu. Taarifa hiyo ikasema wachezaji hao watapelekwa kwenye KAMATI YA NIDHAMU kwa hatua zaidi za kinidhamu.

Mwezi 1 na siku 12 baadae sekretarieti ya klabu ya Simba kupitia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) inatoa taarifa kwamba mchezaji Clatous Chama amesamehewa na anajiunga na wenzie mjini Kigoma. Taarifa inasema kwamba haya ni maamuzi ya KAMATI YA UFUNDI ya Bodi ya Simba ambayo ilipitia maelezo ya Chama na pia uamuzi wa kocha BENCHIKHA kumsamehe mchezaji, Bodi ikaridhia na kusitisha kumpeleka kwenye KAMATI YA MAADILI.

CEO na sekretarieti hawatupi taarifa zinazolingana, wanatuacha na mkanganyiko mkubwa, Chama alipelekwa Kamati ya Nidhamu kwa makosa yake au alipelekwa Kamati ya Ufundi? Kamati ya Ufundi iliyo chini ya Suleimani Haroubu inahusuana nini na nidhamu? Kamati ya Nidhamu ipo chini ya Suleimani Kova, au sekretarieti wameshindwa kutofautisha hizi kamati? Kwanini wapo ofisini kama ndo hivyo, kulikuwa na ulazima gani wa mkanganyiko huu, AIBU. Idara ya Habari inapaswa kuona aibu kwa kutoa vitu vyenye mkanganyiko kwa umma.

Kuna mahali unasoma wanasema Bodi imeridhia na kusitisha kumpeleka KAMATI YA MAADILI, unajiuliza hawa watu vipi? Kamati ya maadili inaingiaje hapo? Lakini pia nimejifunza kumbe tangu waseme wanampeleka kwenye Kamati ya Nidhamu bado alikuwa kwa BENCHIKHA wala kwa Kova hakufika. Anyways, muhimu Chama ameomba radhi amesamehewa ila Sekretarieti ijue namna ya kuhabarisha umma sio kutipika tipika mambo kama hivi amkeni details kwenye Habari na kazi zenu ndo kilakitu fanyieni kazi mnatoa sana boko.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)

SOMA NA HII  IMEVUJAAA....HII HAPA 'LIST' YA MASTAA WAPYA SIMBA....WATAANZA KUSHUSHWA MMOJA MMOJA...