Home Simba SC MAMA..MAMAAH..KWA TIZI HILI LA SIMBA KESHO YANGA ANAKUFA MAPEMA TU

MAMA..MAMAAH..KWA TIZI HILI LA SIMBA KESHO YANGA ANAKUFA MAPEMA TU


NYOTA saba wa Simba wanaandaliwa kuhakikisha mechi ya watani wa jadi kesho Jumamosi, Yanga wanaondoka huku wakiwa vichwa chini kutokana na kipigo ambacho wamewaandalia.

Katika mazoezi makali ya Simba yanayoendelea Uwanja wa Mo Simba Arena Bunju, kocha Didier Gomes amekuwa akikomaa zaidi katika kushambulia na akiwandaa zaidi wachezaji saba.

Wachezaji hao ambao walikomaliwa zaidi katika zoezi la kushambulia ni Luis Miquissone, Clatous Chama, Larry Bwalya na Bernard Morrison ambao walikuwa na kazi mbili.

Kwanza, walitakiwa kuchukua mipira kwa viungo kisha kuwapiga chenga mabeki waliokuwa wanawakaba kina Joash Onyango, Pascal Wawa, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein na Erasto Nyoni.

Washambuliaji hao wakifanikiwa kumpiga chenga beki walitakiwa kufanya mambo mawili – kutoa pasi ya mwisho au kutengeneza nafasi kwa John Bocco, Chriss Mugalu na Meddie Kagere ambao kazi yao ilikuwa kuwafunga makipa Aishi Manula, Benno Kakolanya na Ally Salim. Bocco, Kagere na Mugalu kuna nyakati walifunga ila muda mwingine walishindwa kufanya hivyo kutokana na ubora wa kukaba wa Onyango na Wawa.

Kazi ya pili ilikuwa kama wamempita beki huku Bocco, Kagere na Mugalu wakiwa wamekabwa walitakiwa kufunga wenyewe. Gomes alitumia midoli mikubwa mithili ya watu kisha kuwataka washambuliaji wake kuizunguka na kuipita kama mabeki wa timu pinzani ili kufunga mabao.

Kama ikitokea mchezaji yeyote kati ya saba waliohusika kushambulia akagusa mdoli huyo, maana yake ameshindwa kufanya vile ambavyo Gomes alihitaji na zoezi lilirudiwa.

Kwenye zoezi hilo Gomes alikuwa mkali kama washambuliaji wakishindwa kufunga, kutengeneza nafasi au ikitokea beki amepitwa kwa urahisi na kumpa uhuru mpinzani wake.

Katika zoezi hilo Morrison alikuwa kivutio kwani kuna nyakati alipiga chenga mabeki mpaka hiyo midoli ambayo iliwekwa uwanjani kisha kupiga shuti kali kwa kipa aliyekuwa langoni na kuna wakati alifunga, alitoa nje na mengine yalidakwa.

MILTON, AJIBU NJE

Katika mazoezi hayo Simba waliwakosa wachezaji wawili, Jonas Mkude ambaye bado suala lake linaendelea pamoja na Ibrahim Ajibu.

Ukiachana na wachezaji hao Simba ilimkosa kocha wa wa makipa, Milton Nienov ambaye amekwenda kwao Brazil kwa masuala ya kifamilia ambaye atarejea nchini mara baada ya mchezo na Yanga.

SOMA NA HII  MASHABIKI WARUHUSIWA KUINGIA SIMBA V KAIZERS CHIEFS, SIMBA KUOMBA WENGINE ZAIDI