Home Uncategorized EXCLUSIVE, YANGA WAIGOMEA VODACOM

EXCLUSIVE, YANGA WAIGOMEA VODACOM


Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Fredirci Mwakalebela, umesema hautaweza kuvaa jezi yenye nembo nyekundu ambayo ni ya wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom.

Mwakalebela amefunguka kwa kusema kuwa hawataweza kuvaa jezi hizo kwani hawana utamaduni wa kuvaa rangi hiyo bali kijani na njano pamoja na nyeusi.

Ameeleza uwepo wa hali mbaya kiuchumi kwao usiwe sababu ya kuwafanya wageuke kanuni, taratibu na katiba ya klabu kwani ni jambo ambalo haliwezekani.

Makamu huyo amewaomba TFF kupitia Rais wake, Wallace Karia, wazungumze na Vodacom ili kubadili rangi ya nembo hiyo ndipo wanaweza kuvaa.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAINYOOSHA KMC JAMHURI, MOROGORO