Home kimataifa LIVERPOOL WATAJWA KUWA KWENYE RADA ZA MASTAA KIBAO, TRAORE,MBAPPE

LIVERPOOL WATAJWA KUWA KWENYE RADA ZA MASTAA KIBAO, TRAORE,MBAPPE


WAKATI dirisha la usajili Ulaya likitarajiwa kufungwa leo Agosti 31 usiku, Liverpool inatajwa kuwa katika hesabu za kuwa kwenye anga za za kunasa saini za baadhi ya nyota.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa katika rada hizo ni Saul Niguez ambaye ni kiungo ndani ya Klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania ana umri wa miaka 26 alikuwa anatajwa kuwaniwa pia na Manchester United.

Yupo pia Renato Sanches kiungo anayecheza ndani ya Ligue 1 akiwa katika Klabu ya Lille na ana umri wa miaka 24 alikuwa anatajwa pia kuwaniwa na Wolves.

Kylian Mbappe mshambuliaji wa PSG huyu Real Madrid wanampigia hesabu kali wanashindana katika dau tu kwa sasa na Adama Traore, mwenye miaka 25 akiwa anacheza winga ndani ya Wolves alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Spurs pia.


SOMA NA HII  LIONEL MESSI ASHAWISHIWA KUONGEZA MKATABA BARCELONA