Home news WAKATI HUKU YANGA WALIMUONA KITUKO..SARPONG AWA LULU UARABUNI..KULIPWA TSH MIL 27 KWA...

WAKATI HUKU YANGA WALIMUONA KITUKO..SARPONG AWA LULU UARABUNI..KULIPWA TSH MIL 27 KWA MWEZI


WAKATI Yanga jana ikitambulisha wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao, mshambuliaji wa timu hiyo, Mghana, Michael Sarpong amejiunga na klabu ya Al Nahda ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka miwili huku akikomba mshahara wa dola 12,000 sawa Sh milioni 27 kwa mwezi.

Sarpong alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sport ya Rwanda lakini alishindwa kuisaidia Yanga kwenye eneo la ushambuliaji hali iliyopelekea kuvunjwa kwa mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia.

Akizungumza na Championi Jumatatu, meneja wa mshambuliaji huyo, Mnyarwanda, Alex Kamanzi alisema kuwa tayari mchezaji wake ameshajiunga na Al Nahda baada ya kumalizana na Yanga kufuatia kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

“Sarpong ameshapata timu yupo Saudia Arabia amejiunga na Al Nahda kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachana na Yanga kufuatia kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

“Kitu kikubwa cha kushukuru upande wetu wa kuhakikisha tumepata sehemu ya mchezaji wetu kucheza kwa sababu ndiyo lilikuwa jambo la msingi kutokana na mazingira yalivyokuwa, mchezaji yupo Saudia Arabia kwa sasa ameshakamilisha kila kitu na ameanza maandalizi ya msimu,” alisema Kamanzi.

SOMA NA HII  SIMBA KUINGIZA MIL 2.2 KILA SEKUNDE 60...MO DEWJI AFANYA MAAJABU YAKE...JASHO NA DAMU KWA MKAPA