Home Habari za michezo SIMBA KUINGIZA MIL 2.2 KILA SEKUNDE 60…MO DEWJI AFANYA MAAJABU YAKE…JASHO NA...

SIMBA KUINGIZA MIL 2.2 KILA SEKUNDE 60…MO DEWJI AFANYA MAAJABU YAKE…JASHO NA DAMU KWA MKAPA

SIMBA KUINGIZA MIL 2.2 KILA SEKUNDE 60...MO DEWJI AFANYA MAAJABU YAKE...PATASHIKA NGUO KUCHANIKA

DOKEZO: Tajiri kaweka milioni 200 mezani ambazo kwa hesabu ya kawaida ndani ya dakika 90 kwenye kila dakika watakayokuwa uwanjani watalipwa Milioni 2.2. Hapo bado ule mkwanja wa Rais Samia Suluhu.

SIMBA imekamia kurejea robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ili kuvuta mabilioni ya pesa kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kuhakikisha hilo linatimia vigogo wa Msimbazi wametangaza bonasi mpya kwa wachezaji katika mchezo ujao dhidi ya Horoya ya Guinea.

Tajiri kaweka milioni 200 mezani ambazo kwa hesabu ya kawaida ndani ya dakika 90 kwenye kila dakika watakayokuwa uwanjani watalipwa Milioni 2.2. Hapo bado ule mkwanja wa Rais Samia Suluhu.

Taarifa nyeti kutoka ndani ya Simba Zinasema kuwa Wachezaji wa kikosi hicho Watakaa kikao leo na kesho kuweka mipango mizito pamoja na kutajwa dau hilo na mabosi, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye amesema Wameongea na Mohamed Dewji ‘Mo

Wameongeza bonasi hilo kwenye mechi ijayo dhidi ya Horoya ambapo badala ya Mil 100 sasa ni Mil 200 kama watashinda.

Mkwanja huo ni hamasa kuhakikisha Simba inafuzu robo fainali wikiendi ijayo kwa Mkapa badala ya Kutegemea mechi za mwisho ugenini.

Habari za uhakika ambazo Soka la Bongo Zimetufikia

Tulikuwa tukitoa bonasi ya hadi sh 150 milioni kama wakishinda mechi za ugenini na sh 100 milioni ikitoa sare ugenini huku ushindi kwenye mechi za nyumbani  100 milioni na sare 50 milioni bonasi ambayo katika mechi na Horoya imepanda na sasa ni milioni 200 kama watashinda.

Simba ikikamilisha kila kitu na hapo akaunti za timu hiyo zitapokea zaidi ya bilioni moja kutoka CAF ikiwa ni bonasi ya kufika robo.

CAF hutoa bonasi kwa timu shiriki kuanzia hatua ya makundi ambapo kwa msimu huu timu zote zitazofika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zitapewa kitita cha dola 650,000 ambazo ni zaidi ya Sh 1.4 bilioni za Kitanzania.

Hivyo mabosi wa Simba wanatak mpunga huo ndio maana ikaongeza bonasi kutoka sh 150 milioni kwenye ushindi wa nyumbani kwenda milioni 200, kiasi ambacho kitatangazwa rasmi  leo au kesho kambini.

Lakini mmoja wa vigogo wa Simba amedokeza kuwa dakika za mwisho kabla ya wikiendi dau hilo kupanda zaidi kwani kuna wadau wenye mapenzi na Simba wamejipanga.

Hata hivyo, bonasi hiyo imeongezwa kwa ushindi tu na kama watatoa sare basi sh 50 milioni  na wakifungwa  patupu.

KILA DAKIKA 2MIL
Ukiachana na hesabu ya mgawanyo wa idadi ya wachezaji, fungu hilo lina maana kuwa kila sekunde kwa Simba kwenye mchezo huo itakuwa na jasho na damu, kwani kimahesabu inaonekana kuwa watakuwa na uhakika wa kuingiza sh 37,000 kwa sekunde moja, iwe ya mpira wa kurushwa faulo, mchezaji amedondoka au vinginevyo lakini fedha hiyo itaingia kibindoni kama watashinda.

Lakini pia dakika moja yenye sekunde 60,  itatumika kuingiza  milioni 2,200,000.

Hii ikiwa na maana kuwa kuanzia dakika ya kwanza hadi ya 90 itakuwa muhimu sana kwa timu hiyo kupata fedha na kuweka rekodi.

Simba wakitumia vyema dakika za kipindi cha kwanza ambazo wataingiza shilingi milioni 100, na kipindi cha pili watakusanya milioni 100 nyingine.

Simba imesajili wachezaji 30

Maana yake kila mchezaji atakuwa na uhakika wa shilingi milioni 6.6 kwenye dakika 90 tu za mchezo huo bila kuweka bonasi tofauti ambazo wanaweza kuzipata kutoka sehemu tofauti,

Fedha ambazo zitakazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia Suluhu Hassani kwa kila bao ambalo watafunga ni milioni 5, lakini ukiweka na wadau wengine ilifika milioni 11.

HESABU ZIKO HIVI
Nguvu yote hiyo ina malengo kwani Simba inahitaji kumaliza kazi mapema kwa Horoya kabla ya mchezo wa mwisho wa kundi C itakaporudiana na Raja Casablanca ya Morocco ugenini baada ya mwanzo Mnyama kuchapwa 3-0 nyumbani.

Hadi sasa Simba ipo nafasi ya pili kwenye kundi C na alama sita nyuma ya Raja wenye pointi 12, ambao tayari wamefuzu na kuacha msala wa nafasi moja kwa Simba,

Horoya yenye alama nne na Vipers walio na moja ambao wao hawana nafasi hata kidogo.

Simba ikishinda mbele ya Horoya itafikisha alama tisa ambazo si Horoya wala Vipers haitazifikia baada ya mechi zake za mwisho hata kama zikishinda.

Lakini kama Simba itatoa sare na Horoya itafikisha alama saba na Waguinea hao watakuwa na tano, na mechi za mwisho Simba itacheza na Raja, Horoya watavaana na Vipers ambao hawana cha kupoteza.

Maana yake karata ya Simba ya kwenda robo fainali ipo mkononi mwa Horoya Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa.

Hata hivyo, kama itashindwa kufika robo fainali, Simba haitatoka mikono mitupu kwenye michuano hiyo kwani itapata bonasi ya dola 550,000, zaidi ya sh 1.2 bilioni za Kitanzania ambazo ni mgao wa timu zinazomaliza kwenye nafasi ya tatu na nne kwenye kundi, kutoka CAF, lakini kumbuka tageti ya Simba msimu huu ni hatua ya nusu fainali.

IKO HIVI..
Mshindi wa kwanza na wa pili kwenye kila kundi atafuzu hatua ya robo fainali na kanuni zinaonyesha kuwa kutafuta hatua ya nusu fainali, timu ambayo ilimaliza ya kwanza kwenye kundi itakutana na timu itakayomaliza ya pili.

Kama Simba watamaliza wa pili kwenye kundi lao, watakutana na kati ya vigogo watatu ambao kwa sasa wanaongoza kwenye makundi yao, Mamelodi, Waydad Casablanca au Esperance ya Tunisia na wakishinda hapo ndiyo watakwenda nusu fainali, tusubiri.

SOMA NA HII  RAGE AMPIGA TWISHENI KOCHA SIMBA...AWAFUNDISHA WACHEZAJI NA MAKOCHA... ISHU NZIMA IKO HIVI