Home Ligi Kuu TPBL YABADILI RATIBA NBC PREMIER LEAGUE…MECHI YA SIMBA YAPANGULIWA…YA YANGA YARUSHWA…

TPBL YABADILI RATIBA NBC PREMIER LEAGUE…MECHI YA SIMBA YAPANGULIWA…YA YANGA YARUSHWA…


Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ Imefanya mabadiliko ya Ratiba ya mchezo wa Mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Young Africans dhidi ya KMC FC utakaopigwa Jijini Dar es salaam.

Awali Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa Soka la Bongo ulipangwa kuchezwa Jumatano (Machi 16) majira ya saa moja Usiku, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewana TPLB leo Alhamis (Machi 10) Mchana imeeleza kuwa, mchezo huo umesogezwa mbele na sasa utachezwa Jumamosi (Machi 19), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam saa moja Usiku.

Sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kupisha marekebisho ya miundombinu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, yaliyopangwa kufanyika Februari 15 hadi 18 mwaka huu 2022.

Katika hatua nyingine ‘TPLB’ imeahirisha mchezo namba 142 kati ya Mabingwa watetezi Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania uliokua uchezwa Machi 27, kwenye Uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro, ili kupisha michezo ya kirafiki ya Timu ya Taifa ya Tanzania iliyo kwenye kalenda ya FIFA.

Kwa mujibu wa Taarifa ya ‘TPLB’ imeelezwa kuwa Mchezo huo wa Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania utapangiwa tarehe nyingine.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...PABLO AINGIA BARIDI SIMBA...AIJAZA UPEPO ASEC MIMOSAS MAPEMA...