Home Uncategorized SONSO AJA NA MKWARA YANGA

SONSO AJA NA MKWARA YANGA


BEKI mpya wa Yanga, Ally Mtoni Sonso amesema kuwa alikuwa na ndoto kubwa sana ya kucheza na Yondani na baada ya kusajiliwa na Yanga amesema wapinzani wakae pembeni.

Sonso juzi Ijumaa akiwa nchini Misri na timu ya Taifa ya Tanzania alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa.

Sonso ameliambia Spoti Xtra kuwa, alikuwa na ndoto ya kucheza na Yondani kwani ni beki bora kwake na anaamini kuwa kama wakicheza pamoja hakuna mshambuliaji yeyote wa kumsumbua.

“Yondani ni beki mzuri sana hakuna asiyefahamu hilo na mimi nilikuwa natamani siku moja nicheze naye timu moja kwani kwa uwezo wake mzuri alionao tukicheza wote hakuna mtu wa kutusumbua kabisa,’’ alisema beki huyo.

SOMA NA HII  NAMUNGO FC: UPEPO NI MBAYA KWETU