Home Uncategorized SIMBA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA A-ONE, YAVUNA MAMILIONI

SIMBA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA A-ONE, YAVUNA MAMILIONI

KLABU ya Simba,imeingia mkataba na Kampuni ya A-one kwa ajili ya kutangaza bidhaa yao mpya ya Mo xtra Energy wenye thamani ya Tsh.Milioni 250.

Mkataba huo umesainiwa leo na Meneja Masoko wa A-One, Fatma Dewji na Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ambapo umesainiwa ukiwa mwendelezo wa mkataba wa timu hiyo na kampuni hiyo.

Hii ni mara ya Pili kwa Simba kusaini mkataba na kampuni hiyo ambapo mara ya Kwanza ilikuwa mwaka jana huku fedha za mkataba huo zikipangwa kwenda katika ujenzi wa Uwanja wa timu hiyo uliopo Bunju jijini Dar.

“Kwa niaba ya Simba napenda sana kuwapongeza A-one kwa kuendelea kuithamini klabu yetu kwa kutupatia udhamini huu mkubwa kwetu.

“Tunatambua mkataba wa awali pia ulikuwa na thamani kama hii ya Milioni 250,lakini pamoja na hivyo walitufanyia mambo mengi zaidi ya pesa hiyo hivyo tunajivunia kuendelea nao tena,”amesema Magori.
SOMA NA HII  HASSAN DILUNGA AANZA KUAGA SIMBA