Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI BONGO: BAADA YA KUACHWA YANGA…NTIBAZONKIZA ATAJWA ‘KUNUKIA’ DTB FC…ISHU...

TETESI ZA USAJILI BONGO: BAADA YA KUACHWA YANGA…NTIBAZONKIZA ATAJWA ‘KUNUKIA’ DTB FC…ISHU IKO HIVI..


SAID Ntibanzokiza, aliyekuwa nyota wa kikosi cha Yanga anatajwa kuibukia ndani ya kikosi cha Singida Big Stars ambayo zamani ilikuwa inaitwa DTB.

Timu hiyo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22 ikitokea Championship na msimu ujao wa 2022/23 itakuwa ndani ya ligi.

Habari zimeeleza kuwa timu hiyo ambayo itakuwa na maskani yake Singida huku ikitumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani imefanya mazungumzo na mchezaji huyo.

Saido aliachwa na Yanga rasmi Mei 30 baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumeguka.

Hivyo nyota huyo ataibuka Singida akiwa ni mchezaji huru na ataendelea kuwa ndani ya ligi ikiwa dili lake litafanikiwa.

Nyota huyo mchezo wake wa mwisho kucheza ndani ya Yanga ilikuwa dhidi ya Biashara United uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUMSAJILI MAYELE....AHMED ALLY KAIBUKA NA JIPYA HILI...AGUSIA KUSEPA KWA BALEKE..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here