Home KMC FC KINACHOWASUBIRISHA KMC WASHINDWE KUSAJILI HIKI HAPA

KINACHOWASUBIRISHA KMC WASHINDWE KUSAJILI HIKI HAPA


 UONGOZI wa Klabu ya KMC iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya tano na pointi 48 baada ya kucheza mechi 34 umebainisha kwamba utakamilisha usajili wa majembe ya kazi utakapopata ripoti.

Dirisha la usajili likiwa limefunguliwa tayari timu zimeanza kuingia sokoni kusaka nyota wapya ambao watafanya kazi na timu zao ila kwa KMC wao bado hawajaanza vurugu zao.

Ofisa Habari wa KMC wazee wa pira kodi, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua ni wakati wa usajili lakini watafanya kazi pale watakapopokea ripoti.

“Kwa sasa tupo na tunaendelea kufanya kazi imekuwa ni kawaida yetu kila wakati wa usajili kuwa kimya bila vurugu lakini mwisho wa siku tunafanya usajili mzuri.

“Kinachosubiriwa wakati huu ni ripoti ya mwalimu, hatuwezi kusajili bila kutumia ripoti ambayo kwa sasa bado hatujakabidhiwa ikiwa tayari kila kitu kitafanyika,” amesema Christina.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKITAMBA KUWA NA BIGIRIMANA WAO....PACHA WAKE AIBUKIA KMC ...KUANZA MAJAMBOZI NA IHEFU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here