Home Simba SC KUHUSU AJIB NA NDEMLA KUSEPA SIMBA..,ISHU NZIMA IKO HIVI..GOMEZ AANIKA KILA KITU

KUHUSU AJIB NA NDEMLA KUSEPA SIMBA..,ISHU NZIMA IKO HIVI..GOMEZ AANIKA KILA KITU


SIMBA imekwea pia juzi kwenda Morocco kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa huku Jonas Mkude akitoa mpya baada ya kuwakimbia mashabiki na waandishi wa habari.

Lakini habari ya moto ni kwamba, Said Ndemla na Ibrahim Ajibu bado wapo sana Msimbazi baada ya jana kuafikiwa dakika za mwisho baina ya Kocha Didier Gomes na uongozi kwamba waongezewe mikataba. Ajibu licha ya kuwa hakukwea pia jana, lakini amesisitiza kutofanya kosa lolote la kinidhamu.

Msafara wa wachezaji ni 18, ukiongozwa na Gomes, msaidizi wake Seleman Matola,meneja Patrick Rweyemamu uliondoka jana huku kundi lingine la wachezaji litakaloongozwa na nahodha John Bocco likiondoka kesho.

“Tutaondoka kwa mafungu, leo (juzi) wanaondoka wachezaji 18 na benchi la ufundi la watu 12 na kundi lingine ambalo litakuwa na Bocco an wengine litaondoka Alhamisi.

Wachezaji walioondoka jana ni kipa Aishi Manula, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Beno Kakolanya, Aishi Manula, , Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Hassan Dillunga, Gadiel Michael, Benard Morrison, Clatous Chama, Perfect Chikwende, Shomari Kapombe, Thadeo Lwanga, Rally Bwalya, Jonas Mkude, Joash Onyango na Peter Banda.

Habari zinasema kwamba Chikwende na Kagere wamejumuishwa kwenye kikosi hicho huku uongozi wa juu ukiendelea kuangalia hatma zao kwani wamepanga kuwatoa kwa mkopo muda wowote kuanzia sasa ila hawafikia uamuzi wa mwisho.

Hata Chama nae awali hakuwepo kwenye mipango ya Simba lakini wakaamua asafiri wakamalize dili lake na Rabat hukohuko Morocco.

Mkude atoa mpya

Kiungo mtata, Jonas Mkude ambaye amerejea kikosini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu jana alitoa kali baada ya kuwakimbia mashabiki wachache na waandishi wa habari waliofika kwenye uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere.

Simba iliwasili katika uwanja huo wa Terminal 3 saa 7:25 mchana na wachezaji walianza kushuka na kupita mlango maalumu wa kuingia ndani lakini Mkude na kiungo mwenzake Hassan Dilunga wao walishuka na kupita njia ambayo sio waliyopita wenzao huku kiungo huyo akionekana hana habari na mtu.

SOMA NA HII  HUYU HAPA STARIKA LA KUFUNGA KUTOKA TP MAZEMBE ANAYETAJWA KUTUA SIMBA MSIMU UJAO...NI BALAAHA NA NUSU...

Katika msafara huo wachezaji Kagere, Manula, Kapombe,Chama na Nyoni ndio alioonekana kufuatwa zaidi na mashabiki wachache walioomba kupiga nao picha.

Wakati wachezaji hao wakiombwa kupigwa picha ilikuwa tofauti kidogo kwa winga Benard Morrison ambaye alikaa pembeni na kuonekana mtulivu tofauti na alivyozoeleka kuwa mtu wa vituko.

Morrison baada ya kuingia ndani alitafuta sehemu ya kukaa, huku akiwa na utulivu mkubwa tofauti na wenzake ambao walionekana kuzungumza wawili wawili na kuombwa kupigwa picha.

GOMES NA BANDA

Gomes amesema safari yao ya nchini Moroccco ni kwenda kutengeneza timu yenye ushindani zaidi katika msimu ujao kwa kuhakikisha wanachukua makombe.

“Tunataka kufanya vizuri pia kwenye Ligi ya mabingwa na kusogea mbele zaidi ya pale tulipoishia mwaka jana, tuna kazi ya ziada kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Gomes.

Wakati Gomes akisema hayo alipoulizwa kuhusu wachezaji wake Clatous Chama na Luis Miquissone ambao wanaweza kuondoka akagoma kufafanua.

Akizungumzia usajili wa Peter Banda alisema; “Tumemuona kwenye mechi ya Malawi dhidi ya Tanzania ni mchezaji mzuri na ana umri mdogo ambao anahitaji kukua zaidi.”