Home Uncategorized YANGA YAPANIA KUFANYA USAJILI MKUBWA MWAKA HUU, HAWA HAPA HUENDA WAKATUA

YANGA YAPANIA KUFANYA USAJILI MKUBWA MWAKA HUU, HAWA HAPA HUENDA WAKATUA


UONGOZI wa wana familia ya Yanga ambao umekuwa ukiipa sapoti timu hiyo katika masuala ya usajili kampuni ya GSM umesema kuwa una mpango wa kuleta mchezaji mkubwa msimu ujao ambae atasaini dili jipya kuitumikia Klabu ya Yanga mwaka huu.

Miongoni mwa usajili ambao GSM imefanya ndani ya Yanga ni pamoja na ule wa Bernard Morrison, kiungo mshambuliaji raia wa Ghana.

Mhandisi, Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Uendeshaji GSM, amesema kuwa wapo vizuri na mpango wao ni kuona wanaleta mchezaji makini atakayekuja kucheza ndani ya Yanga.


 “Mwaka huu kutakuwa na tofauti kubwa ya mwaka jana na tutakuja na mpango tofauti kabisa kuhakikisha kwamba jezi ziuzike ikiwemo ya kuleta wachezaji wapya. 

“Tumejipanga kufanya usajili mzuri na ni ahadi yetu kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga kwamba kuna usajili mkubwa utafanyika mwaka huu,” amesema.

Miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwidwa na Yanga ni pamoja na kiungo Ally Niyonzima anayekipiga timu ya Taifa ya Rwanda na Yidah Sven.

SOMA NA HII  PRINCE DUBE NI HABARI NYINGINE NDANI YA LIGI KUU BARA