Home Uncategorized SVEN KWA MABAO AFUNIKA, AIPOTEZA YANGA NAMNA HII

SVEN KWA MABAO AFUNIKA, AIPOTEZA YANGA NAMNA HII


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweka rekodi ya kuongoza kikosi hicho kufunga mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu 2019/20 akiwa ameongoza kwenye jumla ya mechi 11, alishinda 9, sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
Katika mechi hizo 11 Sven ameshuhudia kikosi chake kikifungwa mabao 8 na kufunga jumla ya mabao 26 ambayo ni mengi kuliko yale ya Yanga ambayo imecheza mechi 19 na imefunga mabao 24.
Alianza kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli ambapo mechi ya kwanza alishinda mabao 4-0, KMC 0-2 Simba, Simba 2-0 Ndanda, Simba 2-2 Yanga, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mbao, Simba 3-2 Namungo, Simba 2-0 Coastal Union, Simba 2-1 Polisi Tanzania, Simba 0-1 JKT Tanzania, Mtibwa 0-3 Simba.
Sven alisema kuwa kinachoipa ushindi timu yake ni juhudi za wachezaji kupambana ndani ya uwanja.Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 53 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Lipuli .
SOMA NA HII  KMC WATAJA KILICHO NYUMA YA USHINDI WAO