Home Uncategorized NYOTA HUYU ANAIFUKUZIA REKODI YA AJIBU KIMYAKIMYA

NYOTA HUYU ANAIFUKUZIA REKODI YA AJIBU KIMYAKIMYA


NICOLAS Wadada, beki wa Azam FC amezidi kuwa mwiba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuikimbiza rekodi ya kiungo wa Simba aliyoiweka msimu wa 2018/19 akiwa ndani ya Yanga kwa kutoa jumla ya asisti 17 kimyakimya.
Kwa sasa Wadada ametoa jumla ya asisti saba na ana bao moja akiwa amebakiza 10 kuifikia rekodi hiyo ambayo anaikimbiza mdogomdogo kabla ya kuifikia.
Ajibu kwa sasa ana jumla ya asisti nne ndani ya ligi akiwa na Simba na ana bao moja mguuni alilofunga mbele ya Polisi Tanzania.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema kuwa ana amini kwa majukumu ambayo amepewa nyota huyo atawatengenezea mabao mengi wachezaji naye akipata nafasi atafunga pia.
“Kila mchezaji ana jukumu lake ndani ya timu na Wadada ni mchezaji mzuri, majukumu yake anapewa na anatimiza akipata nafasi anafunga akishindwa atawatengenezea wengine, kikubwa ni ushindi,” amesema.
SOMA NA HII  TAMBWE AWAONYA SIMBA KWA JEMBE JIPYA LA YANGA