Home Uncategorized TAMBWE AWAONYA SIMBA KWA JEMBE JIPYA LA YANGA

TAMBWE AWAONYA SIMBA KWA JEMBE JIPYA LA YANGA


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe ametamba kwamba Yanga wamelamba dume kwelikweli kwa kumsajili beki Mustapha Suleiman huku akiwaambia washambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere na John Bocco kuwa kazi wanayo.

Yanga wamemalizana na Mustapha na kumtambulisha kama moja ya silaha zao mpya ambao watazitumia kwa msimu ujao. Wachezaji wengine ambao wamesajili na Yanga kwa msimu ujao ni Lamine Moro, Ally Ally, Balama Mpinduzi, Maybin Kalengo, Juma Balinya na Abdulaziz Makame.

Tambwe amesema kwamba anawasifu Yanga kwa kumsajili Mustapha kutokana na uwezo mkubwa ambao anao.

“Yanga wamelamba dume kwa kumsajili Mustapha. Ni bonge la beki ambapo naamini kama watacheza na Yondani (Kelvin) basi itakuwa siyo mchezo.

“Ninawaonea huruma washambuliaji wa timu pinzani akina Kagere kwa sababu ninaijua shughuli aliyonayo beki huyo wakati anapokuwa uwanjani,” alisema Tambwe.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YATAJA KILICHOWAKWAMISHA MBELE YA SIMBA