Home Uncategorized AZAM FC YATUMA UJUMBE KWA WAPINZANI WAO COASTAL UNION

AZAM FC YATUMA UJUMBE KWA WAPINZANI WAO COASTAL UNION


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa kikosi kinajipanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Februari 15.

Azam FC inakumbukumbu ya kushinda kwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania huku wapinzani wao Coastal Union wakitoka kulazimisha sare ya bila kufungana na KMC Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa maadalizi yapo vizuri na wanaamini wataendelea kupata matokeo kutokana na aina ya kikosi walichonacho.

“Tupo vizuri na kikosi chetu kinaendelea salama kikubwa ni kuona namna gani tunaweza kupata matokeo mazuri kwa wapinzani wetu kwani nao pia wapo vizuri, mashabiki tunaomba watupe sapoti,” amesema.

Kocha Mkuu wa Azam Arstica Cioaba mkononi ana tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Januari baada ya kuwapoteza Malale Hamsini wa Polisi Tanzania pamoja na Sven Vandenbroeck wa Simba.

SOMA NA HII  SIMBA KUISHIA ROBO FAINALI NI USHAMBA.......YANGA WAJA NA KAULI TATA