Home Ligi Kuu KAGERA SUGAR:TUPO TAYARI KWA MZUNGUKO WA PILI

KAGERA SUGAR:TUPO TAYARI KWA MZUNGUKO WA PILI

[the_ad id="25893"]


 MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa kikosi cha Kagera Sugar amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Tayari Kagera Sugar ipo kambini ikiendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kwenye mwendelezo wa ligi.

Kwenye dirisha dogo Maxime amemuongeza pia nyota wa zamani wa kikosi cha Simba, Yusuph Mlipili ambaye ni beki wa kati.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 ipo nafasi ya 8 na ina pointi 22.

Mecky amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya ligi na tunatambua kwamba ushindani utakuwa mkubwa hivyo nasi tutapambana kupata matokeo chanya.

“Mashabiki wazidi kutupa sapoti ili waendelee kupata burudani kwenye mechi zetu ambazo tutakuwa tunacheza ndani ya dakika 90,” . 


SOMA NA HII  WAAMUZI WATAKIWA KUTIMIZA MAJUKUMU KWA WELEDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here