Home Ligi Kuu KMC YAITEMBEZEA PIRA SPANA KAGERA SUGAR

KMC YAITEMBEZEA PIRA SPANA KAGERA SUGAR


 HASSAN Kabunda, nyota wa KMC leo Februari 20 amepachika mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. 

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo KMC yenye sera ya pira spana imeifunika ile sera ya pira burudani ya Kagera Sugar.

Kabunda ambaye ni winga mzawa alipachika mabao hayo dakika ya 78 na 88 huku lile la ufunguzi likifungwa na Abdul Hilallary dakika ya 16.

Kwa msimu wa 2020/21 timu hizi zimegawana pointi tatutatu ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar ilishinda kwa bao 1-0 lilipachikwa na Yusuph Mhilu.

Leo imekuwa zamu ya KMC kusepana pointi tatu na imefunga mabao matatu ikiwa nyumbani.

Mchezo uliopita kwenye ligi kwa KMC ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC huku Kagera Sugar ikiwa imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga.


SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO NDANI YA NAMUNGO FC NJE YA UWANJA MIEZI MITATU