Home kimataifa NYOTA WA MANCHESTER CITY AGUERO AKUBALI KUTUA BARCELONA

NYOTA WA MANCHESTER CITY AGUERO AKUBALI KUTUA BARCELONA


SERGIO Aguero amekubali dili la miaka miwili kusaini ndani ya Klabu ya Barcelona pale mkataba wake ndani ya Manchester City utakapomeguka mwezi ujao kwa mujibu wa ripoti.

Nyota huyo mwenye miaka 32 ataondoka ndani ya Uwanja wa Etihad baada ya msimu huu kukamilika na anatarajiwa kucheza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mei 29 dhidi ya Chelsea.

Ripoti zimeeleza kuwa raia huyo wa Argentina inaelezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili ndani ya Klabu ya Barcelona ambayo inashiriki La Liga na atapewa mkwanja mrefu ikiwa watashinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na timu yake hiyo mpya.

Pia taarifa zimeeleza kuwa siku chache zijazo nyota huyo atakweda kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha dili lake la kuwa ndani ya Uwanja wa Camp Nou na ataungana na mshikaji wake Lionel Messi ambaye naye anatajwa kuwa ataongeza mkataba.

Aguero inaelezwa kuwa alikuwa analipwa Euro milioni 12 kwa mwaka ndani ya Manchester City hivyo mshahara wake utapanda ndani ya Barcelona.

SOMA NA HII  LIVERPOOL YAHITAJI SAINI YA KIUNGO WA UDINESSE