Home Ligi Kuu IHEFU YAKOMALIA KUBAKI NDANI YA LIGI KUU BARA

IHEFU YAKOMALIA KUBAKI NDANI YA LIGI KUU BARA


 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC amesema kuwa bado wanaimani ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.

Ihefu haikuaza vizuri msimu wa 2020/21 kutokana na kile ambacho mwalimu aliweka wazi kwamba ni kukosa wachezaji wenye uzoefu ndani ya ligi.

Ushindi wake walioupata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji baada ya ubao wa Highland kusoma Ihefu 1-0 Dodoma umewafanya wapande mpaka nafasi ya 12 wakiwa na pointi 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.

Mtupiaji katika mchezo wao uliopita Mei 20 alikuwa ni Andrew Simchimba na alipachika bao hilo dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti.

,Katwila amesema:”Bado tuna kazi kubwa ya kufanya hasa kwa mechi ambazo zimebaki ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa nasi tunapambana ili kupata matokeo chanya,”.

Msimu huu timu nne zinashuka ambapo tayari Mwadui FC ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 30 imeshakata tiketi ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

SOMA NA HII  MBEYA CITY YAGOMEA KUSHUKA DARAJA