Home Simba SC MCHEZO MZIMA SIMBA WALIVYOWATULIZA AFRICAN LYON KWA MKAPA

MCHEZO MZIMA SIMBA WALIVYOWATULIZA AFRICAN LYON KWA MKAPA

 MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho ndani ya ardhi ya Bongo, Simba jana wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon.


Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alishuhudia mabao mawili yakipachikwa na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

Ajibu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi zote 8 ambazo Gomes ameongoza kikosi hicho ambapo ni mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi tatu za ligi,mechi mbili za Simba Super Cup na mechi moja ya Kombe la Shirikisho.

Mabao yote alipachika ndani ya 18 kipindi cha kwanza ambapo dakika ya  9 alipachika kwa kichwa baada ya kipa wa African Lyon Bwanaheri Abdallah kutema mpira wa kona uliokutana na kichwa cha Ajibu.

Bao la pili ilikuwa dakika ya 43 baada ya kipa tena kutema shuti kali lililopigwa na Rarry Bwalya likakutana na mguu wa kulia wa Ajibu na kuwafanya Simba kushinda kwa mabao hayo.

Ni Meddie Kagere atajutia nafasi ya penalti aliyopewa dakika ya 20 kupiga nje kidogo ya lango huku Hassan Dilunga naye nafasi aliyotengeneza dakika ya 38 kwa kumpiga chenga kipa kupiga shuti ambalo halikulenga lango.

Kwa upande wa African Lyon, Pascal Kibangula dakika ya 19 alikosa nafasi ya wazi ya kufunga huku Geofrey Mwashiuya dakika ya 27 akikosa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18. 

Kipindi cha pili mbinu ya African Lyon kusaka ushindi ilikwama baada ya kukutana na ukuta wa Erasto Nyoni na Gadiel Michael ambapo walikota nyavuni bao la tatu kupitia wa Perfect Chikwende kwa pasi ya Miraji Athuman.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPONA.... DILUNGA AVUNJA UKIMYA SIMBA...KUMBE ERASTO NYONI NDIYE CHANZO....