Home Simba SC MFARANSA WA SIMBA LEO KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA KIKOSI CHA KWANZA

MFARANSA WA SIMBA LEO KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA KIKOSI CHA KWANZA


 IKIWA leo kikosi cha Simba kinachonolewa a Kocha Mkuu, Didier Gomes kinashuka Uwanja wa Mkapa kusaka ushindi mbele ya African Lyon, Mfaransa huyo ameweka wazi kwamba atafanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza.

Mchezo wa leo ni hatua ya 32 ambapo ikiwa Simba ama African Lyon itashinda itasonga hatua ya 16 bora na ile itakayoambulia kichapo safari itakuwa imewadia.

Simba ni mabingwa watetezi ambapo waliweza kutwaa taji hili kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Namungo ambayo imetinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, Afrika.

Wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kupumzika leo ni pamoja na Luis Miquissone, Clatous Chama, Aishi Manula,Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Rarry Bwalya na Thadeo Lwanga.

Nyota hao walikuwa na kazi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua ya Makundi mbele ya Al Ahly ya Misri na walishinda bao 1-0 lililopachikwa na Luis.

Gomes amesema:”Hautakuwa mchezo mwepesi kwetu kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi ila tutapambana kusaka matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Mabadiliko yatakuwa makubwa kwenye kikosi cha kwanza lengo ni kuwapa mapumziko wale ambao walicheza mechi za kimataifa kwa kuwa bado tuna kaz ya kufanya kwenye mechi zijazo,” amesema.

Mchezo huo utachezwa leo majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  KUHUSU KUKIPIGA MSIMBAZI MSIMU UJAO...SAIDO NTIBAZONKIZA AFUNGUKA A-Z WALICHOAFIKIANA NA MABOSI...