Home Simba SC MORRISON:- SIWANASEMA NINA ‘BUSHA’…? WAJIANDAE KUKEREKA ZAIDI..!!

MORRISON:- SIWANASEMA NINA ‘BUSHA’…? WAJIANDAE KUKEREKA ZAIDI..!!


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison amefichua kuwa kiwango alichokionyesha katika mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan ni mwanzo kwa kuwa amejipanga kufanya mazuri zaidi bila ya kujali wanaosema vibaya.

Morrison amejiunga na Simba akitokea Yanga kwa mkataba wa miaka miwili lakini amekuwa akikosa nafasi kubwa ya kucheza kama ilivyokuwa Yanga kabla ya Jumatano ya wiki hii kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa Simba Super Cup.

Morrison alisema kuwa kwa upande wake hawezi kuzuia watu kusema lakini anachokiangalia kazi yake anaifanya katika ukubwa gani kwa kuhakikisha timu yake inapata matokeo ya ushindi katika kila mchezo.

“Kikubwa ni kuweka nidhamu na kazi, haijalishi nini kipo mbele au wangapi wanakuongelea kwa sababu nipo hapa kwa ajili ya kazi hayo mengine siyo wakati wake kwa sababu katika soka kuna mambo mengi.“

Lakini kikubwa ninachokiangalia kwa sasa ni kuhakikisha nakuwa bora zaidi ya mchezo uliopita, nahitaji kuwa bora zaidi ya sasa ili kusaidia timu yangu kufikia malengo yake,” alisema Morrison.

SOMA NA HII  FT:GEITA GOLD 0 - 5 SIMBA SC.....KIBU DENIS AMPIGA BUSU CHAMA...SAKHO KAMA MESSI VILEE...