Home Habari za michezo PAMOJA NA KUPOTEA MBELE YA AL AHLY JANA…SIMBA WATOA TAMKO HILI ZITO….

PAMOJA NA KUPOTEA MBELE YA AL AHLY JANA…SIMBA WATOA TAMKO HILI ZITO….

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa licha ya ubora ambao walikuwa nao wakipoteza mbele ya Al Ahly wana nafasi ya kufanyia kazi makosa yao kuelekea mchezo wa marudio Caro.

Mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa, Machi 29 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba walishuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Al Ahly.

Ikumbukwe kwamba ni mchezo wa mkono wa kwanza hatua ya robo fainali kete ya pili inatarajiwa kuchezwa Misri Aprili 5 ambapo hatma ya nani atasonga mbele itafahamika.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: β€œTumepoteza mchezo katika siku tuliyokua bora sana kiwanjani. Nafasi nyingi tumetengeneza nafasi nyingi tumepoteza, Huo ndio mpira.

β€œBado tunayo nafasi ya kuipambania timu yetu katika mechi ya marudiano. Malengo yetu ni yale yale Nusu Fainali. Hakuna kukata tamaa mechi ya marudiano itaamua sisi au wao. Poleni wana Simba vita bado inaendelea,”.

SOMA NA HII  BARBARA AFICHUA KINACHOIBEBA SIMBA