Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZA ‘KUIKANDA’ SIMBA JANA….AL AHLY ‘HAOOO CHAP WASEPA ZAO BONGO’…

BAADA YA KUMALIZA ‘KUIKANDA’ SIMBA JANA….AL AHLY ‘HAOOO CHAP WASEPA ZAO BONGO’…

Habari za Michezo leo

Mabingwa Afrika Al Ahly tayari wameianza safari ya kurejea nchini Misri baada ya kumaliza mchezo wao wa jana dhidi ya Simba.

Kuonesha umuhimu wa mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Aprili 5 mwaka huu, mapema leo timu hiyo ilianza safari ya kurejea nyumbani kwenda kujiandaa na mchezo huo.
7
Mabingwa hao wakihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika wataingia kwenye mchezo wa mkondo wa pili wakiwa na uongozi wa bao 1-0 ushindi waliopata jana Dar es Salaam.

Bao la Al Ahly yenye rekodi ya kucheza fainali nne mfululizo katika misimu mitano iliyopita na kutwaa taji mara tatu, liliwekwa kimiani na Ahmed Koka baada ya mpira uliokolewa na kipa Ayoub Lakred kumkuta katika nafasi nzuri na kutupia nyavuni.

Bao hilo lilitokana na shambulizi la kushtukiza kupitia pembeni na nahodha Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kulambwa chenga na Percy Tau aliyepiga krosi iliyokolewa vibaya na Henock Inonga na kuonekana unaenda nyavuni, lakini Ayoub akauokoa na mfungaji kupigilia msumari.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Al Ahly mbele ya Simba katika mechi tisa walizokutana katika michuano ya CAF tangu mwaka 1985, lakini bado Simba ina nafasi ya kupindua meza katika mechi ya marudiano itakayopigwa jijini Cairo, Ijumaa ijayo itakayoamua timu ya kwenda nusu fainali ya michuano hiyo.

SOMA NA HII  NYOTA SABA WA AZAM FC WAITWA TIMU YA TAIFA