Home Yanga SC MRUNDI YANGA AFUNGUKA SABABU YA FISTON KUTOONESHA MAKEKE

MRUNDI YANGA AFUNGUKA SABABU YA FISTON KUTOONESHA MAKEKE


 FISTON Abdol Razack ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga amekingiwa kifua na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze raia wa Burundi kwa kushindwa kuonyesha makeke ndani ya uwanja.


Nyota huyo ambaye amesaini dili la miezi sita mchezo wake wa kwanza ilikuwa ni dhidi ya African Sports, Uwanja wa Azam Complex alitumia dakika 78 katika mchezo wa kirafiki na mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

Kwenye mchezo huo wakati Mbeya ikipata sare ya kufungana bao 1-1 nyota huyo alitumia dakika 74 na nafasi yake ilichukuliwa na Ditram Nchimbi, alishindwa kuonyesha makeke ambayo mashabiki wake walikuwa wanahitaji.

Kaze amesema kuwa bado hajajenga mazoea mazuri na wachezaji wenzake ndani ya uwanja hivyo atakuwa kwenye ubora wake kwenye mechi zake zijazo, mashabiki wasiwe na mashaka.

“Ni mchezaji mpya kwa sasa bado hajazoea ile mikimbio ya wachezaji wenzake kama ambayo naye hajawazoea, ila nina imani kwamba baada ya muda atakuwa kwenye ubora na atafanya vizuri ndani ya uwanja,” amesema.

Jana, Februari 17, Yanga ilikamilisha kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Maxime Uwanja wa Mkapa na kwenye mchezo wa kwanza msimu huu, Yanga ilishinda bao 1-0, Uwanja wa Kaitaba.

Mchezo wa jana waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 3-3, mchezo ambao umekusanya mabao mengi ndani ya uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21.

Kwenye mchezo huo Fiston hakuwa sehemu ya kikosi hicho cha Yanga inayoongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA SIMBA WALIVYOFINYANGWA JANA...IBENGE AINGIA UBARIDI KUKUTANA NA YANGA CAF...