Home Ligi Kuu MTIBWA SUGAR WATAJA SABABU ZA KUWA NA MWENDO WA KINYONGA

MTIBWA SUGAR WATAJA SABABU ZA KUWA NA MWENDO WA KINYONGA


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amesema kuwa kinachowasumbua wachezaji wake kwa sasa kushindwa kupata matokeo chanya ndani ya uwanja ni kutokuwa fiti kwa ajili ya kupambana.

Mtibwa Sugar kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora imefungashiwa virago na JKT Tanzania ikiwa Uwanja wao wa nyumbani, Jamhuri,Morogoro.

Dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 kisha ngoma ilipofika hatua ya mikwaju ya penalti, Mtibwa Sugar 4-5 JKT Tanzania.

Kwenye Ligi Kuu Bara pia mwendo wake ni wa kinyonga, ikiwa imecheza jumla ya mechi19 ipo nafasi ya 12 na pointi zake ni 23.

Hitimana amesema:”Bado wachezaji hawajawa fiti katika mapambano ndani ya uwanja jambo ambalo linafanya tunapoteza mechi zetu.

“Ila haina maana kwamba hili tatizo litadumu hapana muda wake umekwisha ndio maana tunapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

“Kila kitu kinawezekana na ni muda wetu wa kurejea kwenye ubora wetu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa,”.

Mechi yao ya kwanza mzunguko wa pili ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Jamhuri, ikaambulia kichapo cha kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KOCHA MTIBWA: KILICHOTUPONZA NI KUWAUZIA YANGA BEKI WETU