Home Simba SC RATIBA YA SIMBA KIMATAIFA, UPANDE WA ULINZI BADO TATIZO

RATIBA YA SIMBA KIMATAIFA, UPANDE WA ULINZI BADO TATIZO

 KUNDI A Ligi ya Mabingwa Afrika ni moto wa kuotea mbali kutokana na timu ambazo zipo kwenye kundi hilo kuwa zimewekeza kwenye wachezaji na uimara wa vikosi vyao.

Ndani ya kundi hilo ambalo linatajwa kufuatiliwa na wengi pia ipo timu kutoka ardhi ya Tanzania ambayo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck aliyebwaga manyanga, Januari 7,2021.


Wawakilishi hao wa Tanzania wana kazi kubwa ya kuboresha kikosi chao ili kupata matokeo chanya hasa kwa kuanza na sehemu ya ulinzi ambayo ipo chini ya Pascal Wawa na Joash Onyango ambao ni mabeki wa kati.

 Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba ikishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita, njia ya kutokea kwa wapinzani ilikuwa kwa mwamba Mohamed Hussein,”Tshabalala’ baada ya ule upande wa Shomari Kapombe kuonekana ni mgumu. 

Hali hiyo ilifanya kiungo Luis Miquissone kuongeza nguvu ya kuwa beki kwa kuwa alisababisha faulo moja na kona moja kutoka upande wa Mohamed, hapo Simba wanakazi ya kuboresha zaidi.

Ukitazama ushindani ulivyo pamoja na ratiba yao haitakuwa rahisi kufikia mafanikio bila jitihada, itazame namna ratiba ilivyo:-

Februari 23:-

Simba v Al Ahly 

Al Merrik v AS Vita 

Machi 5

Al Merrikh v Simba

Al Ahly v AS Vita

Aprili 2

Simba v AS Vita

Al Merrick v Al Ahly

April 9

Al Ahly v Simba

AS Vita v Al Merrick 



SOMA NA HII  KUHUSU HABARI ZA UBINGWA MSIMU HUU...AZAM FC KUANZA KUTUMIA MBINU ZA KIJASUSI...